28 Juni 2025 - 17:04
Wananchi wa Iran ya Kiislamu leo hii wameonyesha kwamba damu ya Mashujaa–Kuanzia Makamanda Jasiri na Wanasayansi wa Nyuklia ni Mbegu ya Taifa+ Video_6

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as.) - ABNA- Leo hii umeshuhudiwa mkusanyiko mkubwa na wananchi wa Iran waliojitokeza kwa wingi kushiriki katika mazishi na maziko ya makanda wao wa kijeshi, wanasayansi wa nyuklia, na watoto na wanawake waliouawa kishahidi katika shambulizi la kigaidi la Israel dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.

Wananchi wa Iran ya Kiislamu leo hii wameonyesha kwamba damu ya Mashujaa–Kuanzia Makamanda Jasiri na Wanasayansi wa Nyuklia ni Mbegu ya Taifa + Video

Shambulizi hilo la kigaidi la Israel ndilo lililoibua vita vya siku kumi na mbili baina ya Iran na Israel, ambapo Iran ilichukua hatua kali mno ya kuishambulia kwa makombora hatari yenye teknolojia ya hali ya juu, ambalo israel haikulitarajia na badala yake ili kujiokoa na mashambulizi ya Iran ikaomba Marekani iisaidie kuomba suluhu baina yake na Iran ya kusitisha mashambulizi ya Iran dhidi ya utawala huo. Marekani iliiomba Qatar iingilie kati kwa kuwasiliana na Iran na kuiomba Iran isitishe mashambulizi yake dhidi ya Israel, na kwa sababu uislamu unasema adui akiomba suluhu mkubalie, ndipo Iran ilipositisha operesheni yake ya Ahadi ya Kweli 3, iliyodumu kwa muda wa siku 12 ambazo zilitosha kabisa kuichakaza Israel kila kona kwa kuitwanga katika maeneo nyeti mbalimbali ya kijeshi na kiistratejia, jambo lililoifanya Israel kuchanganyikiwa na walowezi wa kizayuni zaidi ya milioni mbili kukimbilia katika kisiwa cha Cyprus na wengi kukimbilia ulaya walikotokea.

Your Comment

You are replying to: .
captcha